Kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA imetoa taarifa kuhusu Ripoti
aliyokabidhiwa Rais Magufuli leo asubuhi kutoka kwa Kamati iliyopewa
kazi ya uchunguzi.
Kamati imetoa taarifa kuwa kampuni ya ACACIA haijatoa taarifa
kamili(sahihi) ya kiasi cha madini kilichopo kwenye makanikia
yaliyoshikiliwa na kwamba amri ya kuzuia usafirishaji wa makontena yenye
mchanga huo inaendelea kuwepo.
ACACIA bado haijaiona Ripoti hiyo inayosema kuwa kiasi cha madini
kilichopo kwenye makontena hayo yanayoshikiliwa hadi sasa katika Bandari
ya Dar es Salaam ni mara 10 ya kiasi kinachotajwa kwenye nyaraka za
usafirishaji. Bado wanatafuta Ripoti kamili na ufafanuzi zaidi.
ACACIA inasisitiza kuwa huwa inatoa taarifa kamili ya kila kitu chenye
thamani ya kifedha ambacho tunazalisha na huwa wanalipa kodi zote
stahiki kwa kila madini yanayotakiwa kulipiwa.
Wanamalizia kwa kusema watatoa taarifa zaidi kwa wateja haraka iwezekanavyo.
Chapisha Maoni