WAZIRI wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe
akiwakilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Leah Kihimbi amezinduwa bia mpya ya Kampuni
ya Bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL), inayojulikana kama
'Serengeti Premium Lite'.
Akisoma
hotuba ya Waziri Mwakyembe katika uzinduzi huo, Bi. Kihimbi alisema
wizara inaipongeza kampuni ya SBL kwa kuendelea kutangaza utalii wa
Tanzania yaani jina la Hifadhi ya Taifa Serengeti kupitia bia yao.
Alisema Bia mpya ya Serengeti Premium Lite iliyopikwa kisasa
iliyozinduliwa na SBL inaendelea kulitangaza hifadhi ya Serengeti hivyo
kuwataka wananchi wapenzi wa kinywaji hicho kuitumia ili kutangaza nchi.
“Programu
za jamii zinazoendeshwa na SBL katika sekta ya elimu, kilimo na
ujasiriamali zimewezesha vijiji vingi hapa nchini kupata maji safi,
watoto kupata elimu ya juu na mamia ya wakulima kupata masoko kwa ajili
ya kuuza mazao yao ambapo SBL hununua mazao yao kama malighafi
inayotumika kuzalishia bia,” alisema Mwakyembe.
Akizungumza
kabla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh
Mehta alisema SBL, ikiwa ni mojawapo ya kampuni kubwa zinazozalisha bia
hapa nchini, imezindua bia mpya aina ya Lite, ikiwa ni muendelezo wa bia
mama ya Serengeti Premium Lager iliyoko sokoni kwa zaidi ya miaka 20.
“Bia
ya Serengeti Premium Lite inazalishwa kwa namna ya kipekee kwa kutumia
utaalamu wa kisasa wa uzalishaji bia. Ina ladha kamili inayoburudisha
zaidi ya bia za aina ya lite ambazo kwa sasa huuzwa reja reja sokoni,”
alisema Mkurugenzi wa Fedha na Bodi ya SBL, Kalpesh Mehta, wakati wa
hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi huyo, bia hiyo inauzwa kwa Sh.1,500 kwa chupa na
kwamba inatarajiwa kuteka soko na jumuia ya wanywaji wake ambao kwa
kipindi kirefu wamekuwa wakitafuta bia halisi ya Kitanzania. “Pamoja na
kuwa na furaha kubwa usiku huu ambapo tunashuhudia uzinduzi wa biaya
Serengeti Premium Lite, niseme kuwa ni bia halisi ya kitanzania yenye
kiburudisho na ladha nyepesi.
Huu
ni mwitikio wa wateja wetu ambao wamekuwa wakiitafuta bia ya aina hii
kwa muda mrefu. Tuna amini kuwa bia hii ya Serengeti Premium Lite,
ambayo imebuniwa na kutengenezwa na wazalishaji bia (bremasters) wa
kitanzania kwa watanzania, itawaleta wateja wetu pamoja zaidi kadri
watakapo kuwa wakifurahia urithi wetu wa aina hii ya bia”, alisema
Mehta.
Aliongeza
kuwa, “Bia ya Serengeti Premium Lite ina ubora ule ule wa kimataifa
sawa na bia mama ya Serengeti Premium Lager ambayoimepokea zaidi ya
medali 10 za ubora wa kitaifa na kimataifa.”
Chapisha Maoni