0
Watoto wa wawili wa familia moja  wa kijiji cha Moa wilayani Mkinga, mkoani hapa, Kijiti Mohamed na Omari Maazizi (10) wamekufa maji baada ya kuzama katika dimbwi la maji ya mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia jana.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amesema kuwa watoto hao wamekufa maji leo (Jumamosi) mchaka katika kitongoji cha Mwakamba.
Wakulyamba amesema aliyeanza kuzama ni Omari ndipo dada yake akaamua kwenda kumuokoa ambapo hakuweza kufanikiwa, wakazidiwa na
kunywa maji yaliyosababisha kukosa pumzi hivyo kupoteza maisha.
“Watu waliokuwa karibu waliwatoa na kujaribu kuwapa huduma ya
kwanza lakini hawakuweza kufanikiwa sababu walishakuwa
wamekufa,”alisema Wakulyamba.
Ofisa elimu ya Sekondari wa Wilaya ya Mkinga, Omari Kombo amewataka
wazazi kuwa waangalifu kwa watoto katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha kwa sababu maeneo mengi yameharibika.

Chapisha Maoni

 
Top