0











Cristiano Ronaldo ameithibitishia dunia yeye ni mchezaji wa aina yake baada ya kuweka rekodi ya kuwa mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu mitano mfululizo. 
Ronaldo amefunga mabao mawili wakati Real Madrid ikiitwanga Juventus kwa mabao 4-1 na kubeba ubingwa wa Ulaya jana usiku.
Mabao hayo mawili yamemfanya amfikie na kumvuka mpinzani wake, Lionel Messi wa Barcelona ambaye alikuwa na mabao 11.
MISIMU
2017- Mabao 12
2016- Mabao 16
2015-Mabao 10
2014- Mabao 17
2013-Mabao 13.
Mabao mawili ya mchezo huo wa jana yanamfanya Ronaldo aendelee kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye Ligi ya Mabingwa, akifikisha mabao 105 tangu 2003 alipoanza kucheza michuano hiyo akiwa Manchester United ya England.
Na anafuatiwa na hasimu wake mkubwa, Muargentina Lionel Messi mwenye mabao 94 tangu mwaka 2005 akiwa na Barcelona.

Chapisha Maoni

 
Top