Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane akiwa na ndoo ya ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya. |
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane jana usiku ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kulitetea Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya timu yake Real Madrid kuibuka mshindi tena kwa kuipiga Juventus kwa mabao 4-1
Zidane
ameiongoza timu hiyo kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara
ya pili mfululizo. Hivyo, rekodi ya kocha aliyebeba kombe hilo mara
mbili au kulitetea inakwenda kwa raia huyo wa Ufaransa ambaye amewahi
kuzichezea kwa mafanikio Juventus na baadaye Madrid.
Pia Zidane anaendelea kutunza rekodi yake aliyoiweka msimu uliopita akitwaa kombe hilo katika kofia mbili tofauti yaani akitwaa wakati akiwa kama mchezaji na baadae akitwaa akiwa kama kocha.
Pia Zidane anaendelea kutunza rekodi yake aliyoiweka msimu uliopita akitwaa kombe hilo katika kofia mbili tofauti yaani akitwaa wakati akiwa kama mchezaji na baadae akitwaa akiwa kama kocha.
Chapisha Maoni